Audio

Audio | Kapaso Bkp Ft Bob Rudala – Nimekuchagua

  “Nimekuchagua Wewe” ni wimbo wa mapenzi uliotungwa awali mwaka 2004 na Bob Rudala, mmoja wa wasanii na watunzi wakongwe katika muziki wa Tanzania. Wimbo huu umeendelea kuimbwa na kusikika kwa miaka mingi, hadi sasa ukipewa uhai mpya kupitia version ya Singeli ya kisasa na Kapaso BKP, akiwa sambamba na mtunzi wake wa awali Bob Rudala.   Katika toleo hili, Kapaso BKP na Bob Rudala wamerudia chorus ya asili, inayobeba kiini cha ujumbe wa wimbo — kuchagua mpenzi wako kwa dhati — huku verse na melody zikiwa mpya, zikionyesha mabadiliko ya kizazi na ladha ya sasa ya muziki.   Wimbo unaelezea:   Maumivu ya mapenzi Changamoto za maisha kama kukosa kodi, umaskini na maneno ya watu Uamuzi wa dhati wa kuchagua mpenzi wako “wa kufa na kuzikana” Midundo ya Singeli imeufanya wimbo huu kuwa mchangamfu, wa kisasa na wenye nguvu, bila kupoteza uzito wa ujumbe wake wa mapenzi ya kweli. Beat imetengenezwa na Care Beat, kisha kufanyiwa mixing na polishing ya mwisho na Producer Fadhili Chunchu.   Kwa Kapaso BKP, huu ni wimbo wake wa pili mwaka 2026, baada ya wimbo wake wa kwanza wa mwaka huo uitwao “Gundu”. Ushirikiano huu na Bob Rudala ni heshima kubwa na uthibitisho wa kuunganisha vizazi vya muziki wa Tanzania.   Kwa ujumla, Nimekuchagua Wewe ni wimbo unaofaa sana kwa Valentine’s Day, ukiwakumbusha mashabiki kuwa mapenzi ya kweli yanajengwa kwenye uvumilivu, imani na uamuzi wa kuchagua mmoja wako kila siku.   Audio | Kapaso Bkp Ft Bob Rudala - Nimekuchagua #INTRO Care Beat Vinanda Classic Oooh bob rudala Chunchu Eeh   #VERSE Kuna muda na feel maumivu Nashindwa ku vumilia Sitamani tu ufike mwisho wetu Wapi nitaegemea Ajari ya mapenzi naofia kitu Break ikisha nasia Mbele kiza nyuma sitaona kitu Maana nimekuzoea Sisi tulimuomba mungu anapanga Ugumu wa maisha ndo umetujenga Moyo wangu umechagua kukupenda wewee Mabonde na milima tulipanda Kwenye moyo nimejenga sijapanga Nashukuru nafurahi Kupendwa na wewee Ndio maana   #CHORUS Nimekuchagua wewe uwe wangu (Wangu mpenzi) Wangu wa maisha wa kufa na kuzikana Usijali maneno wasemayo (Usijali beibe) Ooh wangu wa maisha wakufa na kuzikana   #HOOK Nakupenda wewe Nakupenda ma mama Nakuhusudu wewe Nakupenda ma mama aayaaa   #INSTRUMENTAL   #VERSE Wengi wanajua kila siku kwetu Imeumbwa ya furaha Tushapitia shida na mengi mabalaa Kila changamoto kwetu zinajirudia Oooh Tushalifeli kodi tukakosa pa kukaa Life lenye ziki nguo zenye viraka Upo kwenye moyo sijutii kukujua My loove   #VERSE Sisi tulimuomba mungu anapanga Ugumu wa maisha ndo umetujenga Moyo wangu umechagua kukupenda wewee Mabonde na milima tulipanda Kwenye moyo wako nimejenga sijapanga Nashukuru nafurahi Kupendwa na wewee Ndo maana   #chorus Nimekuchagua wewe uwe wangu uuh Wangu wa maisha wakufa na kuzikana Usijali maneno wasemayo ooh Wangu wa maisha wakufa na kuzikana   #OUTRO Yoyo yoyo yoyooo Aaayaaa Shiii kapaso hapa Genius from Tanzania Nikiwa na bob rudala    
Download Now
Check Also
Close
Back to top button