Audio | Kapaso Bkp Ft Bob Rudala – Nimekuchagua

 

“Nimekuchagua Wewe” ni wimbo wa mapenzi uliotungwa awali mwaka 2004 na Bob Rudala, mmoja wa wasanii na watunzi wakongwe katika muziki wa Tanzania. Wimbo huu umeendelea kuimbwa na kusikika kwa miaka mingi, hadi sasa ukipewa uhai mpya kupitia version ya Singeli ya kisasa na Kapaso BKP, akiwa sambamba na mtunzi wake wa awali Bob Rudala.

 

Katika toleo hili, Kapaso BKP na Bob Rudala wamerudia chorus ya asili, inayobeba kiini cha ujumbe wa wimbo — kuchagua mpenzi wako kwa dhati — huku verse na melody zikiwa mpya, zikionyesha mabadiliko ya kizazi na ladha ya sasa ya muziki.

 

Wimbo unaelezea:

 

Maumivu ya mapenzi

Changamoto za maisha kama kukosa kodi, umaskini na maneno ya watu

Uamuzi wa dhati wa kuchagua mpenzi wako “wa kufa na kuzikana”

Midundo ya Singeli imeufanya wimbo huu kuwa mchangamfu, wa kisasa na wenye nguvu, bila kupoteza uzito wa ujumbe wake wa mapenzi ya kweli. Beat imetengenezwa na Care Beat, kisha kufanyiwa mixing na polishing ya mwisho na Producer Fadhili Chunchu.

 

Kwa Kapaso BKP, huu ni wimbo wake wa pili mwaka 2026, baada ya wimbo wake wa kwanza wa mwaka huo uitwao “Gundu”. Ushirikiano huu na Bob Rudala ni heshima kubwa na uthibitisho wa kuunganisha vizazi vya muziki wa Tanzania.

 

Kwa ujumla, Nimekuchagua Wewe ni wimbo unaofaa sana kwa Valentine’s Day, ukiwakumbusha mashabiki kuwa mapenzi ya kweli yanajengwa kwenye uvumilivu, imani na uamuzi wa kuchagua mmoja wako kila siku.

 

Audio | Kapaso Bkp Ft Bob Rudala – Nimekuchagua

#INTRO

Care Beat

Vinanda Classic

Oooh bob rudala

Chunchu Eeh

 

#VERSE

Kuna muda na feel maumivu

Nashindwa ku vumilia

Sitamani tu ufike mwisho wetu

Wapi nitaegemea

Ajari ya mapenzi naofia kitu

Break ikisha nasia

Mbele kiza nyuma sitaona kitu

Maana nimekuzoea

Sisi tulimuomba mungu anapanga

Ugumu wa maisha ndo umetujenga

Moyo wangu umechagua kukupenda wewee

Mabonde na milima tulipanda

Kwenye moyo nimejenga sijapanga

Nashukuru nafurahi Kupendwa na wewee

Ndio maana

 

#CHORUS

Nimekuchagua wewe uwe wangu (Wangu mpenzi)

Wangu wa maisha wa kufa na kuzikana

Usijali maneno wasemayo (Usijali beibe)

Ooh wangu wa maisha wakufa na kuzikana

 

#HOOK

Nakupenda wewe

Nakupenda ma mama

Nakuhusudu wewe

Nakupenda ma mama aayaaa

 

#INSTRUMENTAL

 

#VERSE

Wengi wanajua kila siku kwetu

Imeumbwa ya furaha

Tushapitia shida na mengi mabalaa

Kila changamoto kwetu zinajirudia

Oooh

Tushalifeli kodi tukakosa pa kukaa

Life lenye ziki nguo zenye viraka

Upo kwenye moyo sijutii kukujua

My loove

 

#VERSE

Sisi tulimuomba mungu anapanga

Ugumu wa maisha ndo umetujenga

Moyo wangu umechagua kukupenda wewee

Mabonde na milima tulipanda

Kwenye moyo wako nimejenga sijapanga

Nashukuru nafurahi Kupendwa na wewee

Ndo maana

 

#chorus

Nimekuchagua wewe uwe wangu uuh

Wangu wa maisha wakufa na kuzikana

Usijali maneno wasemayo ooh

Wangu wa maisha wakufa na kuzikana

 

#OUTRO

Yoyo yoyo yoyooo

Aaayaaa

Shiii kapaso hapa

Genius from Tanzania

Nikiwa na bob rudala

 

 

Share and Enjoy !

Shares

Leave a Comment

/* */